ZINAZOVUMA:

DAR ES SALAAM: Bei ya mafuta yapaa

Bei ya mafuta Dar es Salaam imepanda kutokana na mafuta...

Share na:

Bei za mafuta ya petroli na dizeli zimepaa nchini mwezi huu wa Aprili 2024 ikilinganishwa na Machi 2024.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, petroli imepanda kutoka Sh 3,163 Machi hadi Sh 3,257 kwa lita, huku dizeli ikiongezeka kutoka Sh 3,126 hadi Sh 3,210.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za mafuta zilizoanza kutumika leo Aprili 3, 2024 ambapo kuna ongezeko la bei kwenye petroli na dizeli huku mafuta ya taa bei ikibaki kama ilivyokuwa Machi 2024.

Taarifa hiyo inasema kwa Dar es Salaam bei ya petroli ni Tsh 3,257 ikiwa ni ongezeko la Sh 94, dizeli ni Sh 3,210 kuna ongezeko la Sh 84, mafuta ya taa bei ni Sh. 2,840 sawa na ilivyokuwa mwezi uliopita.

EWURA imesea kupanda kwa bei hiyo kunachangiwa na kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 3.94 kwa petroli na wasatani wa asilimia 2.34 kwa mafuta ya dizeli, kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kwa asilimia 3.19 kutokana na ongezeko la matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya