Serikali ya Crimea yataifisha mali za serikali na wafanyabiashara wakubwa kutoka Ukraine.
Eneo hilo ambalo lilikuwa ni sehemu ya Ukraine hadi mwaka 2014, limekuwa chini ya Urusi kwa takriban miaka 9 tangu kuchukuliwa.
Spika wa bunge la Crimea Vladimir Konstantinov alisema kuwa mali hizo zilizotaifishwa na serikali yao, zinatarajiwa kupigwa mnada hivi karibuni.
Na kuongeza kuwa tayari walishauza baadhi ya mali kwa mnada, na kujipatia Zaidi ya dola milioni 8.5 za marekani sawa na Shilingi Bilioni 21 za Tanzania.
Katika mali hizo zilizotaifishwa, zipo pia mali za watu wakubwa nchini Ukraine, ikiwe moja ya Raisi Volodymyr Zelensiky wa Ukraine.
Wengi wanaamini kuwa serikali hiyo, inapata msukumo wa kuuza mali hizo kutoka Urusi.
Viwango vya kubadili fedha $1= 2500TZS