ZINAZOVUMA:

CRDB Al Barakah yangara tuzo za GIFA

CRDB Al Barakah yangara katika mkutano na tuzo ya GIFA...

Share na:

Benki ya CRDB kupitia dirisha lake la huduma za benki zinazofata sheria za kiislam Al Barakah (Islamic Window) wametunukiwa tuzo ya ubora duniani.

CRDB Al Barakah imepata tuzo hiyo katika mkutano wa 13 wa Uchumi wa Kiislamu wa dunia (GIFA).

Huduma hiyo za dirisha la benki ya kiislamu CRDB, ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2021 nchini.

CRDB ilishiriki katika mkutano huo kwa uwakilishi wa mkuu wa kitengo cha Huduma za Kiislam, Rashid H, Rashid.

Mkuu wa kitengo cha huduma ya fedha ya kiislamu – CRDB akichangia jambo katika mkutano wa GIFA

Kabla ya tuzo hizo kugaiwa, washiriki wa mkutano huo walijadili mambo mbalimbali katika sharia ya kiislamu kama Fintech, bidhaa za kifedha zenye mrengo huo na bidhaa nyingine kama ufadhili wa halaiki (Crowdfunding), teknolojia ya “Blockchain”, hatifungani zenye utaratibu wa kiislamu (Sukuk) na Wakf.


Pia miongoni mwa mijadala hiyo iliangazia namna gani mfumo wa uchumi wa kiislamu unaoweza kusaidia Afrika katika mambo mbalimbali kama, kukua kwa uchumi, haki za kijamii, utunzaji wa mazingira na hata uwezeshaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Cambridge IFA, imetambua juhudi za kampuni na mashirika mbalimbali ikiwemo CRDB Al Barakah, katika kukuza mfumo wa uchumi wa kiislamu duniani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya