Klabu ya soka ya Chelsea ya nchini uingereza imemfuta kazi kocha wake Graham Potter kufuatia matokeo mabovu ambayo timu imekua ikiyapata.
Kocha huyo aliyepewa kibarua hicho kutokea timu ya Brighton mwaka jana mwezi wa tisa na kusaini kandarasi (mkataba) wa kuinoa Chelsea kwa muda wa miaka mitano.
Potter ameuhudumu Chelsea kwa miezi Saba pekee huku katika michezo yake 31 kama kocha mkuu ameshinda michezo 12, kufungwa michezo 11 na kutoa sare iliyobaki huku akiachwa zaidi ya point 12 katika kinyang’anyiro cha nne bora, “top four”.