ZINAZOVUMA:

Chelsea yafuturisha uwanjani.

Klabu ya Chelsea kutoka ligi kuu ya uingereza imewafuturisha waislamu...

Share na:

Klabu ya Chelsea ya nchini uingereza imewafuturisha waislamu waliokaribu na eneo la uwanja wao wa “Stamford Bridge” ulipo jijini London.

Timu hiyo ilitoa ahadi kabla ya Ramadhani kuanza kuwa ingefuturisha waislamu siku ya jumapili ya tarehe 26 ikiwa ni miongoni mwa jambo jema lenye fadhila linalopatikana ndani ya mwezi huu mtukufu.

Watu mbalimbali walipata kuhudhuria futari hiyo ambayo ilifanyika ndani ya uwanja wao wa “Stamford Bridge”.

Chelsea imekua klabu ya kwanza kutoka ligi kuu ya uingereza kufanya jambo kama hilo.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya