ZINAZOVUMA:

CHAD: Uchaguzi baada ya wimbi la mapinduzi kupita

Raia wa Chad wanatarajia kufanya uchaguzi wa Rais na kuona...

Share na:

Wananchi wa Chad wanatarajiwa kupiga kura siku Jumatatu, miaka mitatu baada ya utawala wa kijeshi kushika madaraka kufuatia kifo cha Idriss Déby.

Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza wa rais katika nchi hiyo ya eneo la Sahel barani Afrika, tangu wimbi la mapinduzi liingie katika nchi hiyo.

Mahamat Idriss Déby amekuwa akihudumu kama rais wa mpito tangu aingie madarakani, baada ya babake Idriss Déby kufariki vitani mwaka Aprili 2021.

Idriss Déby alifariki kwenye machafuko yaliyoanzishwa na kundi la FACT kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya kushika madaraka kwa miaka zaidi ya 30.

Mahamat Déby ameahidi kuimarisha usalama, utawala wa sheria na kuongeza uzalishaji wa umeme ikiwa atapewa nafasi ya kuongoza nchi hiyo kama rais.

Lakini mpinzani wake mkuu amekuwa akivuta umati mkubwa kuliko ilivyotarajiwa kwenye mikutano yake ya kampeni.

Uchaguzi huo utafanyika sanjari na wanajeshi wa Marekani kuondoka kwa muda nchini Chad, ambaye ni mshirika muhimu wa eneo la Afrika Magharibi na Kati.

Eneo hilo la ukanda wa jangwa la Sahara limekuwa na mashambulizi mengi yayayosadikiwa ya kigaidi, na hivyo kuhitajika washirika wa kijeshi kimkakati kama Marekani au Urusi ili kupambana nayo.

Maeneo ya kupiga Kura yatafunguliwa saa 1 asubuhi na kufungwa saa kumi na moja jioni, na watu wapatao milioni 8.5 wamejiandikisha kupiga kura.

Wanajeshi wan chi hiyo wameanza kupiga kura mapema siku ya Jumapili.

Matokeo ya kwanza ya uchaguzi yanatarajiwa kuanza kutoka Mei 21 na matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutoka Juni 5.

Ikiwa hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, itafanyika duru ya pili ya uchaguzi Juni 22.

Tangu alipochukua nafasi ya urais wa muda, Déby ameendelea kuwa karibu na Ufaransa kama mkoloni wa zamani na mshirika wa muda mrefu wa Chad.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya