ZINAZOVUMA:

Viongozi wa Afrika wagomea mkutano na Urusi

Raisi wa Urusi Vladimir Putin amezilaumu NATO na nchi za...

Share na:

Kumekua na sintofahamu kubwa kwa viongozi wa Bara la Afrika kufuatia yanayoendelea duniani. sintofahamu hii imejidhihirisha katika mkutano kati ya Urusi na Afrika.

Uchache wa viongozi wa Afrika katika mkutano huo umesababisha Raisi wa Urusi Vladimir Putin kuzilaumu nchi za Magharibi pamoja na NATO kuwa wamechangia idadi hiyo ndogo ya viongozi wa Afrika katika mkutano huo.

Mkutano huo ni wa pili kati ya Urusi na Afrika unaofanyika huko St. Petersburg, Urusi. Mkutano huo wa siku mbili umeanza leo Alhamisi ya Julai 27, 2023 na utamalizika Ijumaa hii ya Julai 28,2023.

Mkutano huu umelenga kuunganisha juhudi za kuleta amani, maendeleo na mustakabali wenye mafanikio, ambapo Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Comoro, Azali Assoumani, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) wanaendesha mkutano huo kwa pamoja.

Viongozi wakuu 49 kati ya 54 wa serikali za Afrika walihudhuria mkutano wa kwanza uliofanyika Sochi, Urusi mwaka 2019, lakini mwaka huu ni viongozi 17 kutoka Afrika ndiyo wanaoshiriki mkutano wa mwaka huu, idadi ambayo haifiki hata nusu ya walioshiriki mkutano uliopita, uliofanyika kabla ya Urusi kuivamia Ukraine Februari 24, 2022.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya