ZINAZOVUMA:

Burkina Faso imelifungia jarida la Kifaransa la jeune Afrique

Uongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso umelifungia jarida la Kifaransa...

Share na:

Uongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso umelifungia jarida la Kifaransa la Jeune Afrique, linaloandika habari zake nchini humo kwa madai ya kuandika ripoti za uongo zilizoibua wasiwasi na sintofahamu kwa jeshi la taifa hilo.

DW Swahili imeripoti kuwa, taarifa ya jeshi la nchi hiyo iliyotolewa jana jioni, imelishutumu jarida hilo kwa kutaka kulidhalilisha jeshi na kusambaza habari ili kueneza machafuko nchini humo.

Hayo yameonekana katika makala mbili za hivi karibuni zilizochapishwa na gazeti hilo siku nne zilizopita.

Hii ni moja ya hatua kali za karibuni kali zilizochukuliwa dhidi ya gazeti hilo la kifaransa tangu kuingia madarakani kwa utawala huo wa kijeshi nchini humo.

Hata hivyo uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, Burkina Faso pamoja na Ufaransa umezidi kudhoofika.

Jeune Afrique halikuzungumza chochote lilipoombwa kuzungumzia uamuzi huo unaochukuliwa na Kapteni Ibrahim Traore alieingia madarakani kufuatia mapinduzi ya Burkina Faso.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya