ZINAZOVUMA:

BRICS yapanga kuishusha dola

Umoja wa nchi za BRICS umepanga kuja na sarafu mpya...

Share na:

Umoja wa nchi za BRICS katika mkutano wao wa mwezi wa nane wamepanga kuchagua sarafu/pesa mpya watakayoitumia katika biashara zinazounganisha umoja huo.

Sarafu hii mpya ina lengo la kuondoa utawala wa sarafu ya Marekani ambayo ndio inayotumika zaidi duniani.

BRICS imekua na dhamira ya dhati ya kuhakikisha inadidimiza na hata kuondoa nguvu ya sarafu ya Marekani katika biashara lakini pia BRICS imeonekana kuwa mpinzani wa mataifa saba yenye nguvu duniani G7.

Aidha wakati huu kumekua na maombi mengi kutoka nchi mbalimbali kujiunga na umoja huo wa BRICS ambao umeonekana kuwa na nguvu.

BRICS ni unajumuisha nchi za Brazil, Urusi, India, China, pamoja na Afrika Kusini.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya