ZINAZOVUMA:

BOEING kuweka Makao Makuu ya Afrika nchini Ethiopia

Shirika la kutengeneza ndege duniani la Boeing limeichagua Ethiopia kama...

Share na:

Nchi za Kenya, Afrika Kusini, na Ethiopia ambazo zilikuwa zikigombea kuwa mwenyeji wa kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing.

Nchi hizo zilikuwa kwenye orodha ya nchi ambazo shirika hilo la kutengeneza ndege duniani ilizifikiria kuweka makao makuu yake kwa bara la Afrika.

Kampuni hiyo ya Boeing ilichagua kuweka makao yake makuu nchini Ethiopia, na kuyabwaga hayo mengine kutokana na rekodi nzuri ya Usalama wa anga barani Afrika.

Katika maandalizi ya shirika la Boeing kuingia Afrika, limemteua Henok Shawl kuongoza kitengo hicho cha Afrika.

Shawl, ambaye hapo awali aliwahi kuhudumu katika Shirika la Ndege la Ethiopia, alichaguliwa kwa sababu ya uzoefu wake mkubwa kwa mazingira ya Afrika na sekta za anga na mawasiliano.

Kampuni ya Boeing inayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Trilioni 278za tanzania sawa na (USD bilioni 107) hadi mwaka 2024, mwaka jana ilisambaza ndege za kibiashara 528 na kupokea Maombi halisi ya kutengeneza ndege zaidi ya 1,500.

Mwezi Machi mwaka huu Shirika la ndege la Ethiopia liliweka rekodi ya kuwa mteja wa kwanza Afrika kununua Boeing 777X.

Na mwaka jana iliagiza Boeing787 Dreamliners 11 na ndege 20 za Boeing737 Max, kama sehemu ya mkakati wake wa usafiri wa ndege kisasa barani.

Inatazamiwa kuwa sababu ya Boeing kuweka ofisi Afrika, ni matarajio ya kukua kwa mahitaji ya ndege barani Afrika ndani ya miaka 20 ijayo.

Tayari Boeing na Shirika la Ndege la Ethiopia wamesaini Hati ya Makubaliano ya Kimkakati (MoU), ili kuboresha shughuli za zake kama Maendeleo ya Viwanda, Mafunzo zaidi juu ya masuala ya anga, Ushirikiano wa kielimu, na Maendeleo ya Uongozi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya