Amir Sanusi II wa Kano amerudi madarakani, baada ya kutolewa na Gavana wa zamani wa jimbo hilo.
Cheo cha Amir katika jimbo la Kano ni cha kidini na kimila, na anayeshika nafasi hiyo huwa na ushawishi mkubwa kwa jamii.
Gavana Abdullahi Umar Ganduje alimtoa Amir Sanusi kutokana na tofauti za kisiasa, juu ya kurudishwa tena kwa Gavana huyo katika uchaguzi.
Gavana Ganduje alimtoa kwenye cheo hicho mwaka 2020 kwa madai ya kudharau mamlaka, na badala yake zikatengenezwa nafasi tano za mamiri wa Kanda 5 kwenye jimbo hilo.
Katika uchaguzi wa Gavana wa mwaka 2023, Gavana Abba Kabir Yusuf aliahidi kumrudisha Amir Sanusi Madarakani ikiwa atapita.
Na ametekeleza ahadi yake baada ya kupata nafasi ya Gavana wa Kano, pamoja na mahakama kuweka pingamizi juu ya maamuzi hayo.
Amir Sanusi II amesomea uchumi hadi ngazi ya Shahada ya umahiri na amewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria kipindi cha Urais wa Umaru Yaradua na Goodluck Jonathan.
Mbali na uchumi pia amesoma masomo ya dini kama Quran, Sheria, Fiqh na Falsafa, katika chuo cha International University of Africa nchini Sudan.
Baada ya Gavana Yusuf kutangaza kumrudisha madarakani, Mahakama iltoa amri ya kusuia asirudishwe kama Amir baada ya Alhaj Aminu Ado Bayero kupeleka shauri hilo mahakamani.
Alhaj Aminu Ado Bayero (Aminu Babba Dan Agundu), aliteuliwa kuwa Amir wa Kano na
Ingawa amri hiyo ya mahakama ilitupiliwa mbali na Gavana wa Kano na kusema kuwa, “haiwezekani Hakimu wa Marekani akatuzuia umtawaza Amir Sanusi, Sheria zetu hazibadiliki”
Na Katika sakata hilo wananchi wamekuwa na maoni mbalimbali, kuna waliotamani kumwona Muhammad Sanusi akirudi madarakani na wamefurahi kwa hatua ya Gavana kumrudisha.
Na kuna wengine walitamani mbali na kurudishwa kama Amir, lakini wale ma amir watano wabakishwe ili iwe rahisi kufikisha changamoto zao.