ZINAZOVUMA:

Akamatwa kwa kuvunja Sanamu la Kanisa

Mkuu wa Wilaya ya Mjini katika Visiwa vya Zanzibar ametoa...

Share na:

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mjini ambae pia ni Mkuu wa wilaya hiyo Rashid Simai Msaraka amethibitisha kushikiliwa na Jeshi la Polisi kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la abdul Swamad Abbas Ibrahim mwenye miaka 24 kwa tuhuma za kuvunja masanamu katika kanisa la St. Joseph (kanisa la Minara miwili) lilopo Mji Mkongwe Zanzibar

Dc Msaraka ametoa kauli hiyo muda mchachche baada ya kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 3:30 asubuhi ambapo amesema taarifa za awali zinadai kuwa kijana huyo ni mgonjwa wa akili huku akisema kuwa jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na ufatiliaji ili kujua ukweli wa taarifa hizo

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mudrik Soraga amesema serikali haikubalini na vitendo hivyo ambayo vinaashiria kuwepo kwa mifarakano na kuleta taharuki kwa wannachi na wageni wanaotembelea visiwa hivi

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uhifadhi na uendeshaji wa Mji Mkongwe Mhanidis Ali Said Bakari amesema endapo kijana huyo atabainika kuwa sio Mgonjwa wa akili basi ataadhibiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuharibu maeneo ya urithi na historia hasa katika eneo la kanisa hilo kongwe visiwani Zanzibar

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya