ZINAZOVUMA:

Trump ashtakiwa tena kwa makosa mapya

Raisi wa zamani wa Marekani Donald Trump ameshtakiwa kwa makosa...

Share na:

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameshtakiwa kwa makosa ya kupanga njama ya kubatilisha matokeo katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Trump anatuhumiwa kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na kupanga mpango wa kuilaghai Marekani, kuharibu ushahidi na kula njama dhidi ya haki za raia.

Trump mwenye umri wa miaka 77, ambaye anawania tena urais wa Taifa la Marekani amekanusha makosa hayo na kuyaita kuwa ni upuuzi mtupu.

Aidha Trump tayari alikua ameshtakiwa katika kesi nyingine mbili, kwanzi ni kutunza vibaya faili za siri za Marekani wakati wa uongozi wake na kughushi rekodi za biashara ili kuficha malipo ya pesa aliyofanya kwa nyota wa ponografia.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya