ZINAZOVUMA:

Akamatwa kwa kuchora katuni inayomkejeli Waziri Mkuu

Mchoraji katuni maarufu nchini Tunisia amekamatwa kwa kuchora katuni inayomkejeli...

Share na:

Muungano wa wanahabari nchini Tunisia umelaani hatua ya mamlaka nchini humo kumuweka kuzuizini mchora katuni maarufu kwenye taifa hilo.

Kwa mujibu wa taarifa yao Waandishi wa habari nchini Tunisia wametoa wito wa kuachiwa haraka kwa Tawfiq Omrane.

Omrane ameshtakiwa kwa makossa ya kuchora kibonzo kinachodaiwa kumkejeli na kumkosoa Waziri Mkuu wa Tunisia Ahmed Hachani.

Kwa mujibu wa wakili wake, mwanahabari huyo alichukuliwa nyumbani kwake kabla ya kupelekwa katika Ofisi za Usalama wa Kitaifa katika mji wa Mégrine, karibu na mji mkuu wa Tunis, kwa maagizo ya ofisa ya mwendesha mashtaka ya umma.

Omrane anatambuliwa pia kwa uchoraji vibonzo vya kuchekesha kuhusu Rais Kais Saied.

Mamlaka nchini Tunisia imekuwa inatuhumiwa kwa kuendelea kuwazuia wakosoaji wa kisiasa katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya