ZINAZOVUMA:

Afariki akiwavusha bata barabara

Amefariki kwa kugongwa na gari wakati akiwasaidia bata kuvuka barabara ...

Share na:

Mtu mmoja kutoka California nchini Marekani amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akiwasaidia bata kuvuka barabara, polisi wa eneo hilo wamesema.

Casey Rivara (41) aliacha gari lake na kuwavusha bata waliokuwa wanavuka barabara kabla ya kugongwa na gari lililokuwa linaendeleshwa na dereva kijana huko Rocklin, yapata maili 25 (40km) kaskazini mashariki mwa Sacramento.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema Rivara kabla ya kupata ajali hiyo alihakikisha bata hao wamevuka salama barabara kabla ya kugongwa na gari.

“Mwanamume huyo alikuwa anawasaidia watoto wa bata ambao walikuwa wakivuka kwenye makutano ya barabara, ndipo dereva kijana ambaye alikuwa akielekea upande wa mashariki kwenye Stanford Ranch Boulevard, alimgoga,” idara ya Polisi ya Rocklin imesema katika taarifa yake kwa umma.

Ndugu wa marehemu wamesema Rivala alikuwa akiwarudisha watoto wake nyumbani baada ya mazoezi yao ya kuogelea ndipo walipomwona bata na watoto wake wakihangaika kuvuka katika makutano ya barabara.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya