Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Sonko mpinzani wa Rais wa zamani Macky Sall, ni maarufu miongoni mwa vijana wa taifa hilo la Afrika Magharibi, lakini alizuiwa kwenye uchaguzi wa urais wa Machi 24 kutokana na kukutwa na hatia ya kukashifu, hata hivyo alikana kosa hilo.
Wakifanya kampeni kwa pamoja chini ya kauli mbiu “Diomaye ni Sonko,” Sonko aliwataka wafuasi wake kumpigia kura Luteni wake mkuu, Faye, ambaye alishinda kwa zaidi ya 54% ya kura katika duru ya kwanza.
Akizungumza baada ya kuteuliwa, Sonko alisema atamkabidhi Faye orodha kamili ya uteuzi wa mawaziri unaopendekezwa ili aidhinishwe.
“Hakutakuwa na suala la kumwacha (Faye) peke yake kuchukua jukumu hili zito,” Sonko alisema.