Viongozi wa kundi la mataifa ya BRICS Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini wamekutana tarehe 22 Agosti mjini Johannesburg kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kukubali wanachama wapya.
Taifa mwenyeji wa mkutano huo, Afrika Kusini, limesema kuwa nchi Zaid ya 40 zinataka kujiunga na kundi hilo katika siku za hivi karibuni.
Nchi hizi ni pamoja na Iran, Argentina, Cuba, Kazakhstan, Ethiopia, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Venezuela.
Sababu kubwa ya nchi hizo kujiunga na umoja huo ni dhana kwamba uwiano wa mamlaka unaondoka kutoka Magharibi, na nchi nyingi zinazoendelea zinatazamia kupata mamlaka kama nchi za BRICS.