Taasisi ya An nahl trust imefanya mashindano kwa wanafunzi wa sekondari yanayofahamika kama “Ramadhani Quiz Competition” siku ya Jumamosi tarehe 15 Aprili 2023.
Mashindano hayo yalihusisha shule zaidi ya ishirini kutoka katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Dar es salaam, ambapo kila shule ilileta wawakilishi walioshiriki katika mashindano hayo.
Shule ya sekondari ya Mburahati ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki ilifanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ikifuatiwa na Qiblataini nafasi ya pili na nafasi ya tatu ni kutoka shule ya Zanaki.
Washindi hao watatu walipata Tuzo, vyeti, zawadi nyingne pamoja na kiasi cha fedha kwa mshindi wa kwanza kilichotolewa na Mgeni Rasmi Mr Abdallah Albeit ambae ni Mkurugenzi wa kituo cha kujifunzia cha Andalusia, huku shule zote zilishiriki zikitunikiwa vyeti na vitabu kwa wanafunzi.
Mashindano haya ambayo yamekua yakifanyika katika kila msimu wa mwezi wa Ramadhani yanalenga kuongeza chachu ya kujifunza kwa wanafunzi, kwani maswali wanayoulizwa ni yale wanayojifunza darasani, maswali ya dini, na yale ya ufahamu binafsi.