ZINAZOVUMA:

Yanga wapo tayari kwa hatua ya awali klabu bingwa

Klabu ya Yanga imetangaza viingilio vya mchezo wa hatua ya...

Share na:

Klabu ya Yanga imetangaza viingilio vya michezo miwili ya mechi ya awali wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika CAF.

Yanga imesema michezo yote miwili dhidi ya timu ya ASAS Djibouti itachezwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Viingilio katika mchezo huo vitakua ni VIP A Tsh 30000, VIP B Tsh 20000 na mzunguko itakuwa ni Tsh 5000.

Tayari tiketi zimeanza kutolewa makao makuu ya timu hiyo lakini pia zitaanza kusambazwa kwenye vituo vingine mapema iwezekanavyo.

Hayo yamesemwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga ambae pia ametangaza tarehe ya mchezo wa kwanza ambao utakua ni tarehe 20 August, 2023.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya