Mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuanza kuanzia siku ya kesho jumanne ya tarehe 19 Septemba, 2023 huku ajenda kuu zikiwa ni mabadiliko ya tabia ya nchi na mzozo wa Ukraine.
Mabadiliko ya tabia ya nchi na vita nchini Ukraine vinatarajiwa kuangazia pakubwa katika mkutano huo wiki hii wakati ambao viongozi zaidi ya 140 na wawakilishi wa mataifa kutoka kote duniani wakikutana mjini New York kuhutubia kikao cha 78 cha Hadhira Kuu ya Umoja wa Mataifa.
Mjadala huo mkuu unaogusia masuala ya jumla ambao unaanza hapo kesho kufuatia wiki mbili za mikutano, ndiyo tukio linalofuatiliwa zaidi katika kalenda ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa
Mkutano wa mwaka huu utafanyika huku nguvu kubwa ikiwa katika kujadili vita vinavyoendelea nchini Ukraine, mizozo mipya ya kisiasa katika kanda ya Afrika Magharibi na Amerika Kusini.
Lakini pia ugonjwa unaoendelea wa UVIKO-19, ukosefu wa utulivu wa kiuchumi, kuongezeka kwa ukosefu wa usawa na majanga mapya ya asili katika mfumo wa matetemeko mabaya ya ardhi, mafuriko na mioto.