ZINAZOVUMA:

WMO yasema kutakua na ongezeko la joto duniani

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limeeleza...

Share na:

Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO limeekeza kuwa gesi chafuzi za viwandani na matukio ya kimaumbile ya ‘El-Nino’ imetajwa kuwa ni sababu itakayopelekea kuongezeka kwa kiwango cha juu zaidi cha joto duniani kwa miaka mitano ijayo.

Taarifa ya ‘WMO’ imefafanua kuwa kuna uwezekano wa asilimia 66 kwamba wastani wa joto duniani karibu na uso wa dunia kati ya mwaka 2023 na 2027, utakuwa zaidi ya nyuzi joto 1.5°C juu ya viwango vya kabla ya maendeleo ya viwanda.

WMO imefafanua katika taarifa hiyo kuwa kuongezeka kwa joto kunakosababishwa na matukio ya mfumo wa hali ya hewa wa El Nino kunatarajiwa kuendelea katika miezi ijayo. Ongezeko la joto pia limesababishwa na mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na binadamu.

Petteri Taalas Katibu Mkuu wa WMO amesema, Hali hii itakuwa na madhara makubwa kwa afya, uhakika wa chakula, usimamizi wa maji na mazingira. Tunahitaji kujiandaa.

Kwa kawaida, El Niño huongeza viwango vya joto duniani mwaka mmoja baada ya kutokea, katika hali hii, hiyo inamaanisha ni mwaka 2024.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya