Hofu imetanda nchini Niger baada ya kukamilika kwa muda wa wiki moja uliotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wa kurudishwa madarakani kwa Rais Mohamed Bazoum.
Jeshi la nchi hiyo lililochukua madaraka limetoa taarifa kwamba majeshi kutoka mataifa ya jirani yanajiandaa kuishambulia Niger na raia wake huku taarifa hiyo ikiwa haijaweka wazi ni mataifa gani yanayotaka kushambulia.
Katika taarifa hiyo Niger imesema nchi yoyote itakayoingilia kati kinachoendelea itachukuliwa kama muasi na jeshi la Niger halitosita kujibu mapigo.
Aidha katika hali ya kujilinda jeshi la Niger limelazimika kuifunga Anga ya nchi hiyo na kuahidi kutetea na kuilinda vyema nchi hiyo dhidi ya yoyote.