Apple siku ya Ijumaa 19 Aprili, 2024 ilitangaza kuwa, imeondoa mitandao ya WhatsApp na Threads katika App Store nchini China.
Kampuni hiyo ilisema kuwa, imefanya hivyo kwa kufuata agizo la serikali ya Uchina, ambayo inasemekana ilitaja wasiwasi wa usalama wa kitaifa.
Hata zikitolewa Threads na WhatsApp, programu nyingine za Meta, Messenger na Instagram, bado zinapatikana App Store hadi Ijumaa asubuhi huko Uchina, iliripoti Reuters.
Uondoaji huu unaolenga huduma za teknolojia za Marekani kulingana na Bloomberg, unakuja huku serikali ya Marekani ikichukua hatua kuelekea kupiga marufuku TikTok inayomilikiwa na kampuni ya ByteDance ya nchini China.
Wanasiasa wa Marekani, pia, wametaja wasiwasi wa usalama wa kitaifa kama sababu ya kushinikiza Tiktok inunuliwe na asiye Mchina au kupigwa marufuku katika soko la Marekani.