ZINAZOVUMA:

Waziri wa Mambo ya Nje wa China amepotea

Waziri wa Mambo ya Nje wa China amepotea tangu mwezi...

Share na:

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang hajaonekana hadharani tangu mwishoni mwezi uliopita na kuzua tetesi juu ya uhusiano wake na mtangazaji maarufu wa televisheni.

Qin mwenye umri wa miaka 57 ambae ni msaidizi na mwanadiplomasia aliyeaminika na Rais Xi Jinping, aliteuliwa kwenye wadhifa huo mwezi Disemba mwaka 2022, akitokea kwenye nafasi ya balozi wa China nchini Marekani. Qin pia aliwahi kuwa balozi nchini Uingereza.

Mbali na ubalozi, Qin pia amepitia nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP), alijenga jina kwa ujasiri wake katika masuala ya kidiplomasia, hasa mikutano yake na maofisa wa serikali katika nchi za magharibi.

Hali hii si ya kawaida kwa waziri wa mambo ya nje kutoonekana hadharani kwa kipindi kirefu namna hiyo.

Hata hivyo, kuna taarifa zisizo rasmi kwamba waziri huyo amejihusisha kwenye mapenzi na mtangazaji maarufu wa televisheni, Fu Xiaotian (40), ambaye pia ameelezwa hajaonekana tangu waziri huyo alipotoweka

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya