ZINAZOVUMA:

Waziri wa Iran azuiwa kuingia Washington

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezuiliwa kuingia Washington...

Share na:

Marekani imekataa maombi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

ya kutembelea Washington sababu ikiwa ni wasiwasi wa rekodi ya nchi hiyo ikijumuisha na kushikiliwa kwa raia wa Marekani siku za nyuma.

Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollajian, aliripotiwa kutaka kusafiri kutembelea ofisi ya ubalozi baada ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, aliwaambia wanahabari kwamba waliwasilisha maombi yake lakini yalikataliwa na Wizara.

Amesema kwamba hawana jukumu la kuruhusu maafisa wa Iran na mataifa mengine wa serekali kusafiri kwenda New York kwa shuguli za Umoja wa Mataifa, lakini linapokuja suala la kuingia Washington jukumu hilo ni la kwao.

Iran wiki iliyopita iliwaachia raia watano wa Marekani kutoka gerezani kwa kubadilishana na kuachiliwa dola bilioni 6 za Iran kutoka Korea Kusini katika akauti yake ya Qatar.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya