ZINAZOVUMA:

New York yaruhusu adhana isikike kwa jamii

Waislamu jijini New York nchini Marekani wameruhusiwa kuadhin na sauti...

Share na:

Waislamu jijini New York nchini Marekani wameruhusiwa kuadhin kwa sauti kwa kila swala ya Ijumaa na wakati wa swala ya Magharib katika mwezi mtukufu wa Ramadhan pekee bila masharti yoyote.

Uhuru huo umekuja baada ya sheria mpya zilizotangazwa na Meya wa jiji hilo Eric Adams ambapo hapo kabla adhana haikua ikisikika kwa jamii.

Meya huyo amesema kuwa chini ya sheria mpya waislamu hawataitaji ruhusa ya kuwaita waislamu wenzao misikitini kwa ajili ya kufanya ibada.

Aidha imewekwa wazi kuwa jeshi la polisi jijini humo litashirikiana na viongozi wa misikiti na nyumba zote za ibada ili kuhakikisha sheria hiyo mpya inafuatwa.

Meya Adams amesema kutakua na kipimo maalumu cha kiwango cha sauti ambacho kitaruhusiwa kusikika au kufika kwa jamii ili pia isiwakwaze wengine.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya