ZINAZOVUMA:

Waziri Ulega kuanzisha BBT mifugo

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega amesema wizara...

Share na:

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara yake imejipanga kuanzisha programu ya BBT Mifugo katika ranchi ya Mkata kwa lengo la kuwawezesha vijana na wafugaji wengine kufanya ufugaji wa kisasa na wenye tija.

Ulega ameyasema hayo wakati akiongea na Wafugaji wa Kijiji cha Parakuyo wakati alipofanya ziara katika ranchi Mkata iliyopo wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro Jumanne Julai 4, 2023.

“Tumepanga kutengeneza vitalu kwenye ranchi hii kwa ajili ya vijana waliomaliza mafunzo kwenye vituo atamizi na wafugaji wa Mkoa wa Morogoro ambao wanahitaji maeneo ya malisho (Livestock Guest House) kwa ajili ya kufanya unenepeshaji wa mifugo”, amesema.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema kuwa wapo tayari kuunga mkono programu hiyo ili yale malengo ya wizara ya kufanya mageuzi katika sekta ya mifugo mkoani humo yaweze kufanikiwa.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya