ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani akamatwa

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani amekamatwa na maafisa wa...

Share na:

Waziri Mkuu wa zamani wa nchi ya Pakistan Imran Khan amekamatwa na maafisa wa kijeshi nje ya mahakama mjini Islamabad ambapo alikua amefikishwa mahakamani hapo kujibu mashtaka ya ufisadi yanayomkabili.

Imran khan anakana mashtaka hayo yanayomkabili huku akisema kuwa ni uchochezi wa kisiasa.

Aidha ripoti zinasema kuwa Imran Khan alizuiliwa na wanajeshi wenye silaha baada ya kuingia katika eneo la boma la mahakama.

Imran Khan Aliondolewa kama Waziri Mkuu mwezi Aprili mwaka jana na amekuwa akifanya kampeni za mapema tangu wakati huo za uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwaka huu.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya