ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana baada ya shambulio la risasi

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao...

Share na:

Kwa mara ya kwanza tangu litokee tukio la kupigwa risasi, Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico aonekana mitandaoni baada ya kuuguza vidonda vya shambulio la risasi.

Alionekana katika hotuba iliyorekodiwa na kurushwa, kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya jumatano, wiki tatu baada ya jaribuio hilo la kumuua.

Robert Fico katika hotuba yake baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa wiki tatu

Katika hotuba hiyo iliyorushwa kabla ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya, Fico alisema shambulio hilo liliharibu afya yake vibaya na “itakuwa muujiza mdogo nikirudi kazini katika wiki chache zijazo”.

Fico anajiuguza majeraha kadhaa, baada ya kupigwa risasi tumboni wakati akisalimiana na wafuasi wake tarehe 15 Mei katika mji wa Handlova.

Mshambuliaji, wake aliyetambuliwa kama Juraj C mwenye umri wa miaka 71, alikamatwa papo hapo na kushtakiwa kwa jaribio la mauaji ya kukusudia.

Ingawa alionekana yuko katika hali nzuri katika hotuba hiyo, Fico aliahidi kurudi kazini mwishoni mwa Juni au mwanzoni mwa Julai.

Kuhusu Mshambuliaji wake Fico amesema hana chuki na mtu huyo, na hatomfungulia kesi kwani amemsamehe.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya