Waziri Mkuu wa Thailand Pryaut Chan-o-Cha hatogombea tena katika uchaguzi wa marudio na taarifa kutoka katika chama chake imesema kuwa atastaafu siasa rasmi.
Taarifa hiyo imekuja siku mbili kabla ya Bunge la nchini Thailand kukaa kwa ajili ya kupiga kura kumchagua waziri Mkuu mpya baada ya uchaguzi wa mwezi wa tano kuwa na changamoto.
Pryaut mwenye umri wa miaka 69 ameiongoza Thailand kutoka mwaka 2014 akiwa kama kiongozi Mkuu wa jeshi baada ya mapinduzi ya kijeshi aliyoyafanya na kujitangaza kuwa ndio Waziri Mkuu.
Hata hivyo mwaka 2019 ulifanyika uchaguzi na chama chake kilishinda viti vingi Bungeni na kupelekea kuchaguliwa kuwa kiongozi akiongoza seneti ya Bunge.
Katika uchaguzi wa mwezi wa tano Vyama vya upinzani vilipinga na kuokosoa uongozi wa Pryaut alieingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.