Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Augustin Matata Ponyo, ametangaza kuwa atawania urais, wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 20 mwaka huu.
Matata Mponyo, anaugana na wanasiasa wengine kama Moise Katumbi, ambaye pia ameonesha nia ya kuwania urais kupambana na Rais Felix Tshisekedi.
Ametoa tangazo hilo alipokutana na wafuasi wake na kueleza ni kwa nini anataka kuongoza nchi hiyo.
“Tuna mpango kabambe wa kurekebisha serikali na kuifanya kuwa ya kisasa ilikuifanya iwe na ufanisi wa kuishindani na lazima tujenge jeshi bora na jeshi la polisi lenye ufanisi na kuwa na ujirani mwema.” alisema Matata Ponyo.