ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu aingilia kati wafanyabiashara kariakoo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atakutana na wafanyabiashara wa kariakoo...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na kamati ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri wa Sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jumatano May 17,2023.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni-Ikulu Dar es salaam Jumatano May 17, 2023 kwa uratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.

Kwa sasa Serikali inaendelea kuwasihi Wafanyabiashara wa Kariakoo kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.

Kauli ya Waziri Mkuu imekuja mara baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo Dar es Salaam kugoma kufungua maduka leo huku wakitaka kuonana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumueleza kero zao ikiwemo utitiri wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Wafanyabiashara hao wamesema kwamba lengo la kuonana na Rais ni kumueleza juu ya Kodi, ukamatwaji holela na matumizi ya mashine za EFD.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya