ZINAZOVUMA:

Wazazi kupatiwa elimu ya lishe.

Wazazi na walezi wanatakiwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali ili kupatiwa...

Share na:

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Mhe. Sofia Kizigo ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kushirikiana na wataalamu wa lishe ili waweze kupatiwa elimu ya lishe pamoja na huduma mbalimbali zinazohusiana na afya.

Mhe. Kizigo ametoa wito huo leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ambapo amesema lengo la kuwapatia elimu wazazi na walezi ni waweze kushiriki katika kusimamia lishe za watoto wao na kutengeneza kizazi chenye lishe bora kwa taifa la Tanzania.

Akizungumza Mhe. Kizigo amesema maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) hufanyika kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika siku hiyo ambayo utekelezwa kila baada ya miezi mitatu.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya