Katika kuhakikisha usalama wa watanzania waliopo nchini Israel baada ya mashambulizi ya Tel Aviv, Ubalozi wa Tanzania nchini humo umetoa taarifa za awali juu ya usalama wao.
Katika taarifa ya ubalozi imesema kuwa, wamefanikiwa kuwasiliana na wanafunzi takriban 350 kutoka Tanzania.
Na kuongeza kuwa bado kuwa wawili hao ambao inaaminika, walikuwa kusini mwa Israel ambapo kuliathiriwa na shambuliona hawajafanikiwa kuwasiliana nao.
Watanzania hao walienda nchini humo kimasomo, na hao wawili walikuwa katika mafunzo ya vitendo katika sekta ya kilimo biashara.
Balozi wa Tanzania Nchini humo Balozi Alex kalua alisema alipokuwa akiongea waandishi wa BBC kuwa anaamini watanzania hao wawili wapo salama, na wao wanajitahidi kuhakikisha usalama wao.
Takriban raia wa Tanzania 260 wapo nchini humo, kwa mafunzo ya kilimo biashara, yaliyowezeshwa na wizara ya Mhe. Hussein Bashe wa kilimo na Ufugaji.