ZINAZOVUMA:

Israel yauwa wanne kutoka Syria

Wanajeshi wanne wa Syria na wapiganaji wawili wanaoungwa mkono na...

Share na:

Wanajeshi wanne wa Syria na wapiganaji wawili wanaoungwa mkono na Iran wameuawa mapema ya leo Jumatatu 7 Agosti, 2023 na wanajeshi wa Israeli karibu na mji wa Damascus.

Hili limetajwa kuwa shambulio la hivi karibuni la anga kutekelezwa na wanajeshi wa Israel katika mji mkuu wa Syria ulioharibiwa na vita.

Mashambulio hayo ya anga yalilenga vikosi vya serikali ya Syria, na ngome za kijeshi na ghala za silaha zinazotumiwa na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Tehran, kulingana na Shirika la kufuatilia haki za binadamu la Syria.

Wakati wa zaidi ya muongo mmoja wa vita nchini Syria, taifa jirani la Israel limetekeleza mamia ya mashambulio ya anga katika ardhi yake, yakilenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah pamoja na maeneo ya jeshi la Syria.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya