ZINAZOVUMA:

Watanzania watekwa na HAMAS

Watanzania wawili waliokuwa wkaitafutwa na ubalozi wa Tanzania nchini Israel,...
Picha kutoka: BBC

Share na:

Serikali ya Israel kupitia ukurasa wa wizara ya mambo ya nje wa mtandao wa X, imethibitisha kutekwa kwa watanzania wawili waliokuwa nchini humo kimasomo.

Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga miongoni mwa vijana walioenda Israel kwa ajili ya mafunzo ya kilimobiashara.

Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na Serikali ya Israel, zimewahakikishia ndugu wa mateka hao wanafanya juhudi za kuwaachia.

Hadi sasa zaidi ya mateka 230 kutoka nchi takriban 25 zikiwemo Marekani, Argentina, Ufaransa, Nepal, Thailand, Ujerumani South Africa na Brazil.

Hamas imesema kuwa mateka wote wapo salama na wamefichwa katika mahandaki yaliyopo katika Ukanda wa Gaza.

Watanzania hao wamekuwa wakitafutwa tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, punde tu baada ya shambulizi la Hamas dhidi ya Israel.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya