ZINAZOVUMA:

Watalii wafariki nchini India

Zaidi ya watalii 22 wamepoteza maisha nchini India baada ya...

Share na:

Zaidi ya watalii 22 wamefariki baada ya mashua yao kupinduka usiku wa Jana jumapili katika jimbo la Kerala kusini mwa India.

Idadi ya waliofariki inategemewa kuongeza huku juhudi za uokoaji zikiendelea leo Jumatatu na chombo hicho kikitolewa kutoka kwenye maji yenye matope.

Msimamizi msaidizi wa polisi wilaya ya Malappuram Abdul Nazar, amekiambia kituo cha “Reuters” kuwa Idadi kubwa ya watu kupita uwezo wa mashua hiyo ndio ulisababisha mashua hiyo kupinduka.

Kabla ya kupinduka jumapili usiku, mashua hiyo iliripotiwa kubeba zaidi ya watu 50, ambayo ni mara mbili ya uwezo wake.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ametuma salamu za rambirambi kupitia mtandao wake wa Twitter, akisema “ameumizwa sana kwa kupoteza maisha ya watu hao”.


Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya