Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Pindi Chana amewasimamisha kazi watumishi wa Uwanja wa Benjamini Mkapa Uliopo Jijini Dar_es_salaam kufuatia hitilafu ya kuzimika kwa taa za uwanja huo katika matukio mawili ya mchezo wa mpira wa miguu.
Ambapo mchezo mmoja ulikua ni tarehe 28 Machi wa Timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Uganda na mchezo mwingine ni kati klabu ya Yanga dhidi Rivers United kutoka Nigeria hapo Jana.
Watumishi waliosimamishwa kazi ni pamoja na Kaimu meneja wa uwanja Ndg. Salum Mtumbuka, Mhandisi wa Umeme Ndg. Manyori Juma Kapesa, na Afisa Tawala Ndg. Tuswege Nikupala.
Aidha Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Said Yakubu amewasimamisha kazi baadhi wa watumishi ili kupisha uchunguzi wakiwemo Gordoa Nsajigwa, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dkt. Christina Luambano. nao pia wanahusika katika majukumu ya uwendeshaji wa uwanja.