ZINAZOVUMA:

Wananchi: Kituo cha Afya Nyarugusu kimejaa rushwa

Wananchi wa Kata ya Nyarugusu watema nyongo mbele ya Mkuu...

Share na:

Wananchi wa Kata ya Nyarugusu katika Halmashauri ya Geita Mkoani Geita, wamewatuhumu baadhi ya watumishi wa kituo cha afya cha Nyarugusu kuwaomba rushwa wagonjwa anayehttaji matibabu.

Rushwa hiyo imekuwa ikitolewa kama gharama za matibabu bila ya kupewa stakabadhi ya Malipo hayo, na kuwaomba TAKUKURU kuchunguza watumishi hao.

Wakizungumza katika mkutano ulioandaliwa kusikiliza kero za wananchi na hao, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba wamesema kuwa wamechoshwa na tabia za baadgi yao kuwaomba rushwa ndio wapate huduma.

“Kero yangu ya kwanza ni kuhusu huduma zisizokidhi katika kituo chetu cha afya, lakini bado tunaombwa sana hela kabla ya kupewa matibabu” alisema mmoja wa wakazi wa nyarugusu anayefahamika kama Adam.

Na kuongeza “ukienda pale unaumwa chochote utaombwa pesa, mfano mimi kuna mtoto wangu aligombana na mtoto mwingine akachubuka Mkono haka kajitu kakahamia hapa niliombwa hela hapo kama Laki mbili na kitu”

Kwa upande wa Dkt. Maro William ambaye ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita, amethibitisha kuwepo kwa watumishi hao ngazi ya vituo vya afya na kukiri kuwachukulia hatua ikiwemo kuwahamisha vituo vyao vya kazi.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba akiongea na wananchi wa Kata ya Nyarugusu wilayani Geita

”Ni kweli tunakiri kuna changamoto zilijitokeza na hasa ziliripotiwa kipindi cha nyuma, na baadhi ya maamuzi yalipelekea ambaye alikuwa ni kinara taratibu za kisheria juu yake lakini pia kwa uchunguzi ambao ulifanyika kwa wakati huo yaliweza kubainishwa moja kwa moja kwa ushiriki ambao ulikuwepo kwa wakati huo ” Mwakilishi Mganga Mkuu wilaya ya Geita, Dkt. Maro.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashim Komba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Geita, kuchunguza Tuhuma hizo huku akisema hayuko tayari kuona wananchi wakishindwa kuhudumiwa katika Vituo vyao vya Afya na Kumuagiza Mganga Mkuu wa wilaya kukaa na kujadili kukomesha tuhuma hizo haraka iwezekanavyo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya