ZINAZOVUMA:

Wahudumu watatu wasimamishwa kifo cha mjamzito

Wahudumu watatu wa afya kutoka wilaya ya Handeni wasimamishwa kazi...

Share na:

Wahudumu wa afya watatu katika Wilaya ya Handeni, wamesimamishwa kazi kwa kifo cha mjamzito.

mwanamama huyo mjamzito amefariki katika kiftuo cha Afya cha Kabuku, tarehe Novemba 11 mwaka huu 2023.

Bado haijafahamika nini sababu ya kifo hicho, ila inahisiwa kuwa kuwa ni uzembe wa wahudumu.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba, ameunda timu ya kuchunguza kutoka ofisi ya afya ya mkoa.

Taarifa ya kuundwa timu hiyo imetolewa na Mhe. Ummy Mwalimu waziri wa Afya na mbunge wa jimbo la Tanga mjini kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mhe. Ummy pia mabaraza ya kitaaluma kama Baraza la Madaktari Tanganyika, Baraza la manesi na wakunga kuchunguza pamoja na vyombo vingine katika sakata hilo.

Waziri ummy ametoa siku saba tu, za uchunguzi na anataka ripoti ya uchunguzi huo aipate pamoja na mapendekezo kutoka Baraza la madaktari na lile la manesi na wauguzi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,