ZINAZOVUMA:

Wagonjwa waathiriwa na mgomo wa madaktari Kenya

Wagonjwa wakosa huduma nzuri katika hospitali za umma nchini Kenya...

Share na:

Wagonjwa wengi wako katika hali ngumu kwenye hospitali tofauti tofauti hapa Kenya, sababu ikiwa ni mgomo wa madaktari. Mgomo huu unalenga kushinikiza serikali kutekeleza mahitaji ya kuwapatia nafasi za mafunzo ya lazima madaktari zaidi ya 4,000 waliohitimu, kutoa ajira, na kuboresha mazingira yao ya kazi.

Madaktari, ambao walianza mgomo wao siku ya Alhamisi, wanataka pia kurudishiwa pesa za ushuru wa nyumba zilizokatwa kwenye mishahara yao, wanataka mishahara yao ilipwe bila kuchelewa, na serikali ishindwe kutoa makato ya kisheria. Wanataka pia mfumo wa bima ya afya utekelezwe na madaktari wanaofanya kazi chini ya mpango wa afya kwa wote waajiriwe kama ilivyokubaliwa kwenye makubaliano ya mwaka 2017.

Dkt. Davji Atellah, Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari hapa Kenya, KMPDU, amesema kwenye mahojiano na Sauti ya Amerika kwamba mgomo huo utaendelea mpaka pale serikali itakapoonesha nia ya dhati ya kutimiza madai yao.

Licha ya serikali kusema haina bajeti ya kutosha kutekeleza hayo yote, mahakama siku ya Jumatano iliamuru kusitishwa kwa mgomo huo na kuwataka madaktari pamoja na serikali kufanya mazungumzo yenye lengo la kutatua mzozo huo haraka iwezekanavyo.

Tangu mgomo uanze siku ya Alhamisi, wagonjwa wamekosa huduma za matibabu kutoka vituo vya afya vya umma, na wamelazimika kutafuta huduma kwenye zahanati na hospitali binafsi.

Hospitali chache ambazo hazikuathiriwa na mgomo huo zimepokea wagonjwa lakini zikatoa huduma za kiwango cha chini baada ya madaktari kugoma kazi, kama ilivyoshuhudiwa Mombasa.

Akiongea na waandishi wa habari Mombasa, Dkt. Atellah ameeleza kuwa serikali imekuwa ikifanya mazungumzo yasiyo na matokeo na madaktari, na sasa ni wakati wa serikali kutimiza ahadi ilizotoa kwenye makubaliano ya mwaka 2017.

Utekelezaji wa makubaliano ya mwaka 2017-2021, yaliyolenga kutatua uhaba wa madaktari, kuongeza mishahara, kuboresha mazingira ya kazi, kuwapandisha vyeo madaktari, na kuhakikisha vifaa vya matibabu vinapatikana, pamoja na kutekeleza mfumo wa bima ya afya, umekuwa tatizo kubwa kutokana na kusita kwa serikali.

Madaktari mara kwa mara wamelalamika kuhusu nyongeza ndogo ya mishahara, ucheleweshaji wa mishahara, makato yasiyoeleweka kisheria na bima ya afya. Pia wamelalamikia uhaa wa madaktari, ukosefu wa vifaa vya kazi, mafunzo ya ziada, kupandishwa vyeo, na haja ya kuwa na ajira za kudumu pamoja na pensheni.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya