ZINAZOVUMA:

Wafanyabiashara Marekani kuwekeza kuikarabati Ukraine

Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema wawekezaji wa Marekani wapo...

Share na:

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema amekutana na wajasiriamali na wafadhili wa Kimarekani wakati wa ziara yake ya wiki nzima nchini Marekani.

Zelenskiy amesema kutokana na mikutano hiyo, majadiliano ya fursa za uwekezaji nchini Ukraine, yalijadiliwa.

Zelenskyy amesema wafanyabiashara ambao alikutana nao ni pamoja na Michael Bloomberg, Larry Fink, na Bill Ackman ambao walikua tayari kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuikarabati Ukraine baada ya vita vyake dhidi ya Russia.

Kupitia mtandao wa Telegram Zelenskiy aliambatanisha na picha za mkutano wake akaandika kwamba wafadhili na wajasiriamali wa Marekani wamemthibitishia kuwa wapo tayari kufanya uwekezaji mkubwa nchini humo mara baada ya kumalizika kwa vita na kupewa uhakika wa usalama.

Katika ziara yake ya Marekani na Canada wiki iliyopita, Rais Zelenskyy ameendelea kusisitiza umuhimu wa msaada wa kijeshi na kifedha kwa Kyiv, katikka juhudi za kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya