ZINAZOVUMA:

Waasi wa zamani nchini Mali wavaa gwanda kurudi tena uwanjani

Wapiganaji wa kutoka kikundi cha waasi kutoka Azawd nchini Mali,...
Waasi wa Zamani wa CMA (Coordination of Azawad Movement)

Share na:

Kikundi cha waasi wa zamani nchini Mali kijulikanacho kama Umoja wa Harakati za Azawad “Coordination of Azawad Movement”, kimetangaza kuwa sasa ndio wakati wa vita na serikali ya kijeshi.

Eneo limekumbwa na machafuko wiki za hivi karibuni, hali ambayo imesababishwa na kuondolewa kwa vikosi vya Misheni ya kulinda amani kutoka Umoja wa Mataifa (MINUSMA).

Kikundi hicho cha waasi ambacho ni muunganiko wa makundi mbalimbai ya Tuareg yenye kudai uhuru au utawala, iliwaomba wakazi wote wa azawad kuchangia juhudi ya mapambano hayo.

Kikundi hicho kilifanikiwa kuwakusanya watu katika kuunga mkono mapambano hayo kwa mitandao ya kijamii, kama ambavyo mapinduzi na machafuko mengi yaliratibiwa barani afrika.

Katika taarifa za kikundi hicho zilizosambazwa mitandaoni, ilisemwa kuwa “lengo ni kulinda nchi na kurudisha udhibiti wa eneo lote”.

Huku taarifa za waasi hao zikiwa na anuani ya “Jeshi la Taifa la Azawad”, zilikuwa zikiwatahadharisha raia kuwa mbali na wapiganaji wa Wagner.

Hatua hii ya waasi hao imekuja baada ya habari kuzagaa kuwa, Utawala huo wa kijeshi umesaidiwa mno na wapiganaji hao wa Wagner.

Mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2015 kati ya waasi hao na serikali ya Mali, upo mashakani kutokana na hali ya vurugu inayoendelea kaskazini mwa nchi hiyo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya