ZINAZOVUMA:

Waamuzi sita wafungiwa kisa Vinicius Junior

Shirikisho la soka nchini Hispania na kamati ya ufundi ya...

Share na:

Shirikisho la Soka la Hispania na Kamati ya Ufundi ya Waamuzi imewatimua waamuzi sita wa VAR kufuatia kumuonesha kadi nyekundu mchezaji wa Real Madrid, Vinícius De Oliveira maarufu kama ‘Vini Jr’ wakati akikutana ubaguzi wa rangi.

Vinicius alikuwa sehemu ya mchezo wa La Liga kati ya Real Madrid walipopoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Valencia Jumapili.

Winga huyo wa Brazil awali alikabiliana vikali na wafuasi wa Valencia, ambao walidaiwa kumbagua Vinicius wakiwa kwenye jukwaa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kofi Hugo Duro baada ya kuchezewa rafu na hivyo kuzua kejeli kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.

Akitumia mitandao ya kijamii baada ya mchezo huo, Vinicius alichapisha taarifa ya kulaani vitendo vya wafuasi hao, na kutochukuliwa hatua kutoka kwa La Liga.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya