ZINAZOVUMA:

Vyama saba vyaungana kushinda uchaguzi

Vyama saba vya upinzani Afrika Kusini vimeungana ili kushinda uchaguzi...

Share na:

Muungano wa vyama saba vya kisiasa nchini Afrika Kusini umesaini makubaliano ya ushirikiano yanayolenga kukiondoa chama tawala cha ANC katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2024.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, iwapo vyama hivyo vitashinda katika uchaguzi huo, vitafanya kazi kwa pamoja na kugawana nyadhifa mbalimbali za Wizara na viti vya ubunge.

Pia wanalenga kukizuia chama cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema kuingia madarakani.

Makubaliano hayo yanakuja wakati huu nchi hiyo ikikabiliana na hali mbaya ya uchumi, ufisadi, ukosefu wa ajira na mzozo wa nishati ambao haujawahi kutokea nchini humo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema ANC iko hatarini kupoteza viti vingi vya wabunge kwa mara ya kwanza tangu Afrika Kusini iingie kwenye demokrasia mwaka 1994.

Hata hivyo kambi hiyo mpya bado haijaamua ni nani atasimamishwa kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya