ZINAZOVUMA:

Viongozi wa Afrika kutafuta suluhu mabadiliko tabia ya nchi

Viongozi wa Afrika wamekutana nchini Kenya kujadili na kutafuta suluhu...

Share na:

Wakuu wa nchi za Afrika wamekutana nchini Kenya kwa ajili ya mkutano wa kilele wa tabia ya nchi barani Afrika, ambapo watajadili mtazamo wa bara hilo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkutano huo unaofanyika Nairobi ni wa kwanza barani Afrika ambao umelenga kuja na mpango wa pamoja wa kuwasilisha kwa viongozi wengine wa dunia katika mkutano wa COP 28 wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa baadaye mwaka huu.

Katika siku tatu zijazo, wajumbe katika mkutano huo watazingatia mtindo mpya wa ufadhili ili kusaidia serikali kupunguza utoaji wa hewa ukaa.

Rais wa Kenya William Ruto amesema Afrika inapaswa kuwa sehemu ya suluhisho la ongezeko la joto duniani, badala ya kuwa mwathirika.

“Kwa muda mrefu sana tumeliona hili kama tatizo. Ni wakati wa kugeuza na kuangalia kutoka upande mwingine,” aliwaambia wajumbe wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya