Siku ya jumapili wapiganaji wa RSF nchini Sudan wameshambulia makazi na kuteka hospitali kuu katika eneo hilo, hali iliyosababisha maelfu kukimbia makazi yao.
Vikosi hivyo vya Msaada wa Haraka vya kijeshi vilifanya mashambilizi kwenye miji vya Jebal Moya, kisha mji wa Singa katika jimbo la Sennar.
Vikosi hivyo vya RSF vilikutana na upinzani wa jeshi la Sudan katika kijiji cha Singa na kusabisha watu elfu 57,000 kukimbia makazi yao kutokana na majibizano yao ya risasi.
Vikosi hivyo vilisheheni silaha za kivita ikwemo magari yenye bunduki za kiotomatiki katika mashambulizi ya Singa, klomita 300 kutoka Khartoum makao makuu ya nchi hiyo.