ZINAZOVUMA:

Uwanja wa ndege wa Mwanza utakuwa wa Kimataifa

Serikali ya Tanzania imeweka wazi mpango wake wa kupanua uwanja...

Share na:

Serikali ya Tanzania kupitia imetangaza nia ya kuufanya uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa wa kimataifa. Mpango huo wa serikali umesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mhe. Stanslaus Mabula mbunge wa Nyamagana.

Mpango huo unalenga kuwaondoa zaidi ya watu 1000, walio karibu na uwanja huo.

Mwanzo ilitegemewa kuwa eneo litakaloathiriwa ni mita 700 kutoka katika mipaka ya sasa, na watakaoathiriwa na mpango huo watalipwa fidia.

Inatazamiwa kuwa mpango wa sasa wa kuoneza eneo la uwanja utaathiri takriban watu 1400, katika kata 5 ikiwemo ya Shibula na Bulyanhulu kuguswa katika mkoa huo wa Mwanza.

Mpango huo wa kukifanya kiwanja hicho kuwa cha kimataifa utahusisha kuongeza eneo la uwanja pamoja na kupanua miundombinu ya uwanja.

Mbali na kupandisha hadhi uwanja huo pia serikali ina miradi kadhaa ya kutengeneza au kukarabati viwanja vya ndege. Miradi hiyo ipo katika mikoa mbali kama uwanja wa Dodoma na wa Msalato, Tabora, Shinyanga, Sumbawanga, Kigoma, Iringa, Songwe pamoja na Arusha.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya