Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema maandalizi ya makubaliano baina ya serikali kati ya Moscow na Burundi kuhusu nishati ya nyuklia ya kiraia yako katika hatua yake ya mwisho.
Lavrov aliyasema hayo Jana baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Albert Shingiro mjini Bujumbura.
“Mwongozo wa nishati ya nyuklia tayari umetiwa saini kati ya Rosatom, Shirika la Nishati la Jimbo la Urusi na washirika wake wa Burundi” Lavrov alisema.
Alisema pande zote mbili zimejitolea kushirikiana katika matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.
Nchi hizo mbili zilitia saini mkataba wa mmwongozo wa nishati ya nyuklia mwezi Novemba mwaka jana, ambapo Urusi ilikubali kuisaidia Burundi kuanzisha mitambo ya atomiki.
Kabla ya kuondoka kwake kuelekea Msumbiji, Waziri Lavrov alikutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye kwa mazungumzo zaidi ya pande mbili.