Kutokana na sintofahamu baina ya Urusi na Mataifa ya Magharibi, Rais Putin amesema kuwa kuna uwezekano wan nchi yake kurudi katika silaha za nyuklia.
Nchi hiyo ya Ulaya Mashariki, iliacha majaribio ya silaha za nyuklia, zaidi ya miongo mitatu iliyopita.
Rais Putin ametoa tamko siku ya alhamisi na kusema kuwa “Urusi haihitaji kubadili msimamo wake juu ya silaha za nyuklia, na atakayeshambulia Urusi ataangamizwa na makombora ya nyuklia”.
Pia Kiongozi huyo wa taifa lenye kuleta usawa wa nguvu dhidi ya Magharibi aliongeza kuwa, watajiondoa katika mkataba wa kuzuia majaribio ya silaha za nyuklia duniani.
Kwani Marekani amesaini mkataba huo na bado anafanya majaribio, hivyo hata nchi yake haijachelewa kufanya kama marekani.
Putin anaamini kuwa hakuna mtu duniani mwenye akili timamu na kumbukumbu nzuri atajaribu kuishambulia urusi kwa silaha za nyuklia.
Tamko hili la Putin juu ya Nyuklia nchini humo limekuaj kama jibu kw aswali la mwanasayanzi Sergei Karaganov, anayeamini juu ya silaha za nyuklia.
Rais Putin aliyasema hayo katika moja ya mikutano ya Klabu ya majadiliano ya Valdai.